Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda S.Burian (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha na timu ya wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), waliofika kueleza mikakati ya Mamlaka kuhakikisha tarehe mosi Julai wakulima wanaanza kununua mbolea katika maeneo yao ikiwa ni maandalizi ya msimu wa kilimo 2023/2024. Kushoto kwake kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku kutoka TFRA Louis Kasera