Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
TFRA YAPONGEZWA NAMNA INAVYOJITOA KUTUMIKIA UMMA
20 Jun, 2025
TFRA YAPONGEZWA NAMNA INAVYOJITOA KUTUMIKIA UMMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania imepongezwa kwa kushiriki katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma. 

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli na Katibu mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Selemani Mkomi walipotembelea banda la Mamlaka leo tarehe 19 Juni, 2025.

Akizungumza na waoneshaji Katibu Mkuu Mweli, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)kuhakikisha kuwa kila mkulima anayefika katika banda anapata huduma ya kusajiliwa kwenye mfumo wa kidijitali wa pembejeo za kilimo ili kuwawezesha kunufaika na  mbolea za ruzuku  zinazotolewa na Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Huku Katibu Mkuu, Mkomi akieleza kufurahishwa kwa namna Mamlaka imejitokeza ili kushiriki kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa maonesho hayo. 

Ameeleza kuwa jitihada  zilizooneshwa na  Mamlaka zinadhihirisha dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.