Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
TFRA kwa Ufupi

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeanzishwa kwa Sheria ya Mbolea na. 9 ya mwaka 2009.

Sheria hii hutekelezwa kupitia kanuni zifuatazo: -

  • Kanuni za Mbolea za mwaka 2011 (Fertilizer Regulations, 2011) na marekebisho ya mwaka 2017 (Fertilizer (Amendment) Regulations, 2017).
  • Kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer (Bulk Procurement) Regulations, 2017).

Taasisi hii ipo chini ya Wizara ya Kilimo na ilianza kutekeleza majukumu yake tangu Agosti 2012. Mamlaka inasimamiwa na bodi ya wakurugenzi na majukumu yake ya kila siku yanasimamiwa na mkurugenzi mtendaji.

MAJUKUMU YA TFRA

1. Kusimamia na kudhibiti ubora wa mbolea nchini.

  • kusajili mbolea
  • kufanya ukaguzi wa ubora wa mbolea katika mnyororo wa tharnani.

2. Kudhibiti utengenezaji, uingizaji na biashara ya mbolea nchini.

  • Kusajili, kutoa leseni, na kutunza kumbukumbu za waten­genezaji na wauzaji wote wa mbolea.
  • Kutoa vibali vya watengenezaji, waagizaji, wasambazaji wa mbolea nchini na wauzaji wa mbolea nje ya nchi.
  • Kusimamia bei za mbolea nchini.
  • Kuunganisha wauzaji na wanunuzi wa mbolea nchini ili kuhakikisha kwamba mbolea inayotosheleza inapatikana kwa wakati.

3. Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na taasisi zingine juu ya masuala yanayohusu sera za usimamizi na udhibiti wa ubora na biashara ya mbolea.

4. Kushirikiana na asasi za ndani na nje ya nchi zinazoshughu­likia mbolea katika kuhakikisha mbolea inamfikia mkulima katika ubora unaokubalika na bei nafuu.

5. Kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuelimi­sha Umma juu ya matumizi sahihi ya mbolea.

 

Mbolea Day