TAARIFA KWA UMMA: KUFUNGIWA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO NCHINI
TAARIFA KWA UMMA KUFUNGIWA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO NCHINI |
Hivi karibuni, Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ilifanya ukaguzi na kubaini udanganyifu unaofanywa na baadhi ya kampuni/mawakala wa mbegu na wadau wengine wasio waaminifu wanaouza mbegu zisizothibitishwa ubora na TOSCI. Hali hiyo inaweza kusababisha wakulima kununua mbegu ambazo hazina ubora na kusababisha hasara kwa wakulima na kuhatarisha usalama wa chakula nchini.
Hivyo basi, wafanyabishara wafuatao wamefungiwa kufanya biashara ya mbegu mpaka itakapoamuliwa vinginevyo.
Na |
Jina |
Namba ya Usajili |
Wamiliki/Wakurugenzi |
1 |
Aghahumbi Co. Limited |
SD/663 |
Omary Mussa Nkwarulo |
Sikujua Issa Kahere |
|||
Aghahumbi Omary Nkwarulo |
|||
2 |
Lauria Gwindevya |
SD/2426 |
Lauria L. Gwindevya |
Vilevile, Wamiliki na Wakurugenzi wa kampuni hizo hawataruhuisiwa kufanya biashara ya pembejeo nchini.
Aidha, kwa kuwa leseni ya biashara ya pembejeo inahusisha mbegu, mbolea na viuatilifu, taarifa inatolewa kwamba usajili/leseni zilizotolewa kwa kampuni hizo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) zimefungiwa kwa kipindi chote cha utekelezaji wa agizo hili.
Taarifa za kufungiwa kwa kampuni hizi zitawasilishwa pia kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zifutiwe leseni zao za biashara.
Kupitia tangazo hili, waagizaji, wazalishaji na wasambazaji wa pembejeo wanakumbushwa kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote ili kuepuka mkono wa sheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa hati za usajili/leseni ya kufanya biashara zinazohusiana na uuzaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo nchini.
Imetolewa tarehe 30/11/2024 kwa idhini ya:
Mkurugenzi Mkuu Mkurugenzi Mtendaji Mkurugenzi Mkuu
TOSCI TFRA TPHPA
Kwa taarifa zaidi:
Tembelea ofisi za TOSCI Morogoro.