Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Mbolea za ruzuku zinapatikana nchi nzima kupitia kwa mawakala (Agrodealers) wa mbolea.
Mkulima atatambua kuwa mbolea ni ya ruzuku kwa kuangalia maneno “MBOLEA YA RUZUKU” yalioandikwa kwenye mfuko wa mbolea.
Mkulima anaweza kuthibitisha kuwa taarifa zake zimesajiliwa kikamilifu kwa kupokea ujumbe wa uthibitisho (SMS) baada ya kukamilisha usajili au kuhuisha taarifa.
 Ndio wakulima wasio na simu janja wanaweza kuhuisha taarifa zao kupitia Afisa Ugani aliyepo karibu ili awasaidie kuhuisha taarifa zao kwenye mfumo kwa kutumia kishikwambi.
Ndiyo mkulima anaweza kubadilisha taarifa zake muda wowote.
Hapana hakuna muda maalum kuhuisha taarifa ni muda wowote.
Ukipoteza namba ya mkulima piga simu kwenye kitengo cha huduma kwa wateja TFRA 0800110153 au 0800110154 hakikisha una taarifa za muhimu za awali kama kitambulisho namba ya simu ili uweze kurejeshewa namba yako ya mkulima.
Mkulima anatakiwa awe na nambe yake ya mkulima na taarifa zake za awali za shamba kama eneo la shamba, aina ya zao analolima na mahali lilipo shamba.
Mkulima analipia sehemu ya gharama si bure kabisa.
 Bei za ruzuku ya mbolea zinapatikana kwenye website ya TFRA ambayo ni www.tfra.go.tz