UWASILISHAJI WA MAHITAJI YA KUINGIZA MBOLEA NCHINI AINA YA DAP NA UREA KUTIPITIA MFUMO WA UNUNZI WA PAMOJA - BPS
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) inawaalika Wafanyabiashara wa Mbolea, Vyama vya Ushirika na wadau wote katika Tasnia ya Mbolea na Sekta ya Kilimo kwa ujumla kuwasilisha mahitaji ya uingizaji wa mbolea aina ya DAP na Urea itakayouzwa kwa wakulima chini ya Mpango wa Ruzuku ya Mbolea kwa msimu wa 2024/2025.
Mahitaji yatajumuishwa na kuingizwa nchini kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) kwa mujibu wa Kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja za Mwaka 2017. Tafadhali wasilisha nakala ngumu ya mahitaji pamoja na dhamana ya benki (kwa kutumia violezo (templates) vya kuwasilisha mahitaji na dhamana ya benki (Bank Guarantee) vinayopatikana katika tovuti ya www.tfra.go.tz.) kwenye ofisi za TFRA au tuma kwa barua pepe kupitia info@tfra.go.tz na nakala kwa bps@tfra.go.tz kabla au ifikapo Jumatatu tarehe 11 Novemba, 2024 saa 10:00 jioni.
Angalizo: Dhamana halisi ya benki (Original Bank Guarantee) lazima iwasilishwe kwa nakala ngumu kabla au ifikapo siku ya mwisho ya kuwasilisha mahitaji.
TFRA itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea bora kwa wakati, bei himilivu na masharti rafiki ya ulipaji.
MKURUGENZI MTENDAJI
MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA TANZANIA (TFRA)
KIATALU NA. 15471, 1 MTAA WA KILIMO, JENGO LA KILIMO I,
SIMU. +255 222 861 939;
BARUA PEPE:info@tfra.go.tz
DAR ES SALAAM, TANZANIA