TAARIFA KWA UMMA: MAREKEBISHO YA BEI ELEKEZI ZA MBOLEA YA CAN NA SA
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ina jukumu la kutoa bei elekezi kwa wafanyabiashara wa mbolea nchini kwa mujibu wa kifungu cha 4(1)(u) cha Sheria ya Mbolea ya Mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea za Mwaka 2011 kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017.
Katika kutekeleza jukumu lake la kisheria, TFRA imefanya marekebisho ya bei elekezi za mbolea ya CAN na SA kwa kuzingatia hali ya soko. Marekebisho hayo yanaanza kutumika tarehe 9 Februari, 2026 (Bei zinapatikana kwenye tovuti ya TFRA www.tfra.go.tz na kwenye mfumo wa ruzuku ya pembejeo). Wafanyabiashara wa mbolea wanatakiwa kuuza mbolea hizo kwa bei elekezi au chini yake.
Aidha, TFRA inatoa wito kwa Mamlaka zote katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoa ushirikiano katika usimamizi wa uzingatiaji wa bei elekezi na utekelezaji wa mpango wa ruzuku kwa ujumla ili kufikia azma ya Serikali ya kuongeza tija katika uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima kupitia kilimo.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA TANZANIA (TFRA)
Februari 9, 2026
