DC KINGALAME AWAASA WAKULIMA KUNUNUA MBOLEA KUPITIA MFUMO RASMI
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale , Grace Kingalame, amewataka wakulima kununua mbolea kupitia mfumo rasmi uliowekwa na serikali ili kuepuka kununua mbolea nje ya bei elekezi.
Akizungumza katika Viwanja vya Nyamuhongolo jijini Mwanza, DC Kingalame amesema mfumo huo utawawezesha wakulima kupata mbolea bora , hivyo kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.
Amesema serikali imeweka mifumo ya udhibiti ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo salama na bora, hivyo kuwataka wakulima kuwa makini na kufuata utaratibu rasmi wakati wa ununuzi wa mbolea.
Kwa upande wake, Afisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Godwin Vedastus , amesema ukaguzi na udhibiti wa mbolea unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha mbolea zinazouzwa sokoni zinakidhi viwango na sinauzwa ndani ya bei elekezi.
Ameongeza kuwa wakulima wanapaswa kushirikiana na mamlaka kwa kutoa taarifa pindi wanapouziwa mbolea nje ya mfumo wa ruzuku.
