MAFUNZO YA BIASHARA YA MBOLEA –MKOA WA IRINGA MJINI, UKUMBI WA UMAKI, TAREHE 27 NA 28 AGOSTI 2026: OFISI YA TFRA DODOMA IMEANDAA
19 Aug, 2026
MAFUNZO YA BIASHARA YA MBOLEA – IRINGA MJINI
Ofisi ya TFRA Dodoma inawatangazia na kuwakaribisha wadau wote kushiriki katika Mafunzo ya Biashara ya Mbolea yatakayofanyika:
📍 Mahali: Ukumbi wa UMAKI, Iringa Mjini
📅 Tarehe: 27 na 28 Agosti 2026
🕑 Muda: Saa 2:00 Asubuhi
Mafunzo haya yanawalenga:
-
Wanaotaka kuanzisha biashara ya mbolea
-
Wafanyabiashara wa mbolea
-
Vyama vya Ushirika
-
Wafanyakazi wa maduka ya mbolea
-
Wafanyakazi wa maghala ya mbolea
Tunawakaribisha wote kujifunza kuhusu taratibu, kanuni na mahitaji muhimu ya kuanzisha na kuendesha biashara ya mbolea kwa usahihi.
OFISI YA TFRA DODOMA
Karibu ujifunze, uelewe na uanzishe biashara sahihi ya mbolea!
