BEI ELEKEZI KWA MBOLEA ZA KUPANDIA NA KUKUZIA KWA MSIMU WA KILIMO 2025/2026 (Toleo la 25)
11 Sep, 2025
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) inajukumu la kutoa bei elekezi kwa wafanyabiashara wa mbolea nchini kwa mujibu wa kifungu cha 4(1)(u) cha Sheria ya Mbolea ya Mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea za Mwaka 2011 kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017.
Katika kutekeleza jukumu lake la kisheria, TFRA imefanya mapitio ya bei elekezi kwa aina kumi na moja (11) za mbolea ambapo aina kumi (10) ni mbolea zinazoingizwa kutoka nje (DAP, UREA, CAN, SA, NPKs, MoP, NPK Tobacco na TSP) na aina moja (1) ni mbolea inayozalishwa ndani ya nchi (Hakika Avomax).
Bei elekezi zitaanza kutumika tarehe 10 Septemba, 2025 (Bei zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Kilimo; www.kilimo.go.tz, na TFRA; www.tfra.go.tz). Lengo la kufanya mapitio na kutangaza bei elekezi ni kuhakikisha kuwa mbolea inauzwa kwa bei inayoendana na gharama halisi za soko. Wafanyabiashara wa mbolea wanatakiwa kuuza mbolea hizo kwa bei elekezi au chini yake.