Kufanya ukaguzi wa mbolea na visaidizi vya mbolea
Ukaguzi kwa ajili ya Udhibiti ubora wa mbolea
Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Mbolea, TFRA itakagua au kuwezesha ukaguzi wa mbolea au visaidizi vya mbolea kwa ajili ya kujihakikishia ubora.
Katika ukaguzi mbolea au kisaidizi cha mbolea itakaguliwa, itachukuliwa sampuli na kufanyiwa uchambuzi kwa ajili ya kudhibiti ubora.