Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
MAFUNZO
MAFUNZO

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) inaendesha mafunzo kwa mtu yeyote binafsi au mwakilishi wa kampuni anayejihusisha au anayekusudia kujihusisha na biashara ya mbolea. Mafunzo ni sharti ambalo lipo kwa mujibu wa Sheria ya Mbolea Na. 9 ya Mwaka 2009, ambayo inaelekeza kwamba wafanyabiashara wote wa mbolea lazima wapatiwe mafunzo yanayohusiana na biashara ya mbolea. Mafunzo haya yanatolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) bila gharama yoyote.

Mafunzo ya wafanyabishara wa mbolea yanaratibiwa na Ofisi ya makao makuu pamoja na kanda zilizopo Nchini kama ifuatavyo:

  1. Kanda ya mashariki: Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara
  2. Kanda ya Kaskazini: Arusha, Manyara, Kilimanjaro, na Tanga
  3. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini: Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, na Katavi.
  4. Kanda ya Ziwa: Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga
  5. Kanda ya kati: Tabora, Dodoma, Singida, Kigoma.