Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Karibu

Bw. Joel Laurent

Mkurugenzi Mtendaji

Kwa niaba ya Bodi Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), ninayofuraha kukukaribisha katika tovuti yetu ambapo unaweza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.

TFRA ilianzishwa kwa Sheria ya Mbolea namba 9 ya mwaka 2009 na kuanza kutumika Agosti 2012 kwa madhumuni ya kuweka masharti ya udhibiti wa utengenezaji,  uingizaji, usafirishaji, usambazaji na matumizi ya mbolea za kilimo.

Tangu kuanzishwa kwa TFRA, jitihada za makusudi zimefanyika ili kuweka mazingira mazuri ya kazi yanayounga mkono mamlaka ya kitaasisi yaliyotolewa na Sheria na Kanuni zake.

Kwa kujibu mahitaji ya wateja wetu na kuboresha utoaji wa huduma, tovuti mpya itatoa huduma kwa wateja masaa ishirini na nne katika wiki(24/7) duniani kote. Tuna uhakika kuwa kuwepo kwetu kwenye wavuti kutaongeza thamani katika suala la utoaji wa huduma kwa ufanisi na kwa wakati, nahivyo kupata mrejesho wa maoni kutoka kwa wadau wetu.

Ni imani yangu kuwa tovuti hii ni jukwaa la  kuelimisha umma kwa ujumla, ambapo machapisho mbalimbali, picha na video mbalimbali kuhusu mamlaka zitapatikana kwa urahisi kwa ajili ya na matumizi ya umma.

TFRA imejizatiti katika maono yake ya "Mbolea Bora kwa Wakulima Wote kwa Uendelevu wa Kilimo" kwa kuhakikisha wakulima kote nchini wanapata mbolea bora na nafuu kwa maendeleo endelevu ya kilimo.          

 

Mbolea Day