Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Usajili wa Wafanyabiashara wa Mbolea na maeneo wanayo fanyia biashara(premises)
Usajili wa Wafanyabiashara wa Mbolea na maeneo wanayo fanyia biashara(premises)

Kwa mujibu wa kanuni za Mbolea za mwaka 2011, ghala au duka la kuhifadhia mbolea linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;

 1. ENEO
 • Ghala linatakiwa liwe mbali na maeneo yanayoweza kutokea mafuriko na pia liwe mbali na vyanzo vya maji.
 • liwe mbali na dampo ama shughuli zozote zinazojihusisha na uteketezaji wa taka kwa njia ya moto; ilikuepusha uwezekano wa mlipuko ghalani na kuyeyuka kwambolea kwani joto ghalani linatakiwa liwe kati ya 50c - 30 0c
 • Liwe pia mbali na maeneo yenye vyanzo vya uchafuzi wa mazingira mfano sehemu wanapo choma tairi, sehemu wanapojihusisha na shughuli za kokoto ilikuzuia uwezekano wa vumbi na moshi kuingia gharani.

2. SAKAFU

 • Ghala iwe imeinuka kutoka usawa wa ardhikwa cm 60 ili isiruhusu maji kuingia na kutoka nje, sakafu inatakiwa iambatane na lamp yenye slope 10 % ilikuwezesha magari ya kubeba mizigo kuingia na kutoka ghalani pia kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu kuingia na kutoka ghalani Sakafu iwe ngumu isiyo na mipasuko ili isiruhusu unyevu kupanda kutoka chini ya sakafu

3. KUTA

 • Kuta za ghala zijengwe kwa kutumia malighafi imara zisizo shika moto na zilizo ngumu kiasi cha kuzuia hali ya hewa ya nje inayoweza kuharibu ubora wa mbolea iliyotunzwa ghalani. (sound wall)
 • Ukuta uwe na nguzo katikati ili kuongeza uimara wa jengo.
 • Kuta zisakafiwe na kupakwa rangi nyeupe kwa ndani,
 • Mfumo wa umeme uwe umesukwa vizuri kutosababisha janga la moto.

4. PAA

 • Ghala liwe limeezekwa kwa malighafi isiyoruhusu maji ya mvuakuingia kutoka juupaa lisiwe na matobo kama inavyoonekana hapo Kenchi za paa ziwe za chuma ili kuongeza uwazi na uimara

5. HEWA

 • Ghala liwe limeezekwa kwa malighafi isiyoruhusu maji ya mvuakuingia kutoka juu
 • paa lisiwe na matobo kama inavyoonekana hapo
 • Kenchi za paa ziwe za chuma ili kuongeza uwazi na uimara

6. MILANGO

 • Ghala liwe na milango mikubwa ya kuingiza na kutolea mbolea (first in and First out) na kuwe na milango ya dharula

7. MWANGA

 • Liwe na mwanga wa kutosha kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na baadhi ya bati ziwe zina bati zinazoruhusu mwanga ndani ya stoo au ghala

8. USAFI

 • Ghala linapaswa kuwa safi muda wote ili kuzuia vumbi kuchanganyika na mbolea

9. MFUMO WA KUTOLEA MAJI

 • Linapswa kuwa na mfumo thabiti wa kutolea maji wakati wa mvua. Mifereji ya kutolea maji ya juu wa kati wa mvua (down pipe) ziwe na uwezo wa kubeba maji yote ya paa na lisiwe na matobo