Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
HUDUMA ZA MAABARA
HUDUMA ZA MAABARA

Mamlaka ina maabara ya kisasa ambapo inatoa huduma za uchambuzi wa sampuli mbalimbali kwa kutumia mashine za kisasa na wataalam wabobevu. Huduma zifuatazo zinatolewa na Maabara ya Taifa ya Mbolea Tanzania:

1. Uchambuzi wa virutubisho vya mbolea

  • Kuchambua virutubisho vikuu (Naitrojeni, Fosforasi, Potasiamu – NPK)
  • Kupima virutubisho vya ziada (Kalsiamu, Magnesiamu, Salfa)
  • Kupima virutubisho vidogo (Zinki, Boroni, Chuma, Manganisi n.k.)

2. Uchambuzi wa Kimaabara wa Sifa za Mbolea

  • Unyevunyevu wa mbolea
  • Umumunyifu wa mbolea
  • Ukubwa na usawa wa chembechembe (granules)
  • Uzito na msongamano wa mbolea

3. Ushauri wa Kitaalamu

  • Ushauri wa kitaalamu kutokana na matokeo ya uchambuzi
  • Mapendekezo ya kuboresha ubora wa mbolea

4. Uchambuzi wa udongo

  • Kiwango cha Asidi au Alkali (pH)
  • Virutubisho vya udongo
  • Organic matter
  • Cation exchange capacity
  • Electrical Conductivity of soil.

5. Upimaji wa sampuli za maji

6. Upimaji wa sampuli za tishu za mimea