Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Maafisa Ugani kugawiwa Vishikwambi, POS kurahisisha usajili, upimaji afya ya udongo
08 May, 2024 09AM:15:00PM
Dodoma
PR

Uzinduzi wa Ugawaji wa Vishikwambi na POS Kwa Maafisa Ugani Kilimo na Mawakala wa Pembejeo za Kilimo umefanyika Mtumba, Jijini Dodoma.

Akizindua ugawaji huo, Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema, Wizara imenunua vishikwambi 3500 pamoja na POS vitakavyorahisisha usajili wa wakulima katika mifumo ya ugawaji wa pembejeo za kilimo na upimaji wa afya ya udongo.

” Wizara tumeazimia kuhakikisha kuwa miradi ya kilimo inatekelezwa ipasavyo ili kuweza kumnufaisha mkulima na kufikia lengo la Serikali la kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 10 ifikapo 2030 huku tukiwa tumefikia lengo la ukusanyaji wa shilingi bilioni 2.3 ya mauzo ya mazao katika nchi za nje.”

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent ameeleza kuwa, kwa sasa kuna ongezeko la uzalishaji wa mbolea kwa viwanda vya ndani ambao umefikia asilimia 11 kwa mwaka 2024 kutoka asilimia 6 mwaka 2021.

Maafisa Ugani kugawiwa Vishikwambi, POS kurahisisha usajili, upimaji afya ya udongo