LESENI
Mamlaka inatoa huduma ya kusajili na kutoa leseni kwa wafanyabiashara wote wa mbolea nchini ikiwa ni takwa la Sheria ya Mbolea Na. 9 ya mwaka 2009. Huduma hii ni muhimu katika kuimarisha na kuhakikisha udhibiti wa ubora wa mbolea katika mnyororo mzima wa thamani.
Wafanyabiashara wote wanaokusudia kufanya biashara ya mbolea wanapaswa kuwasilisha maombi ya leseni kwa kufuata hatua hizi:
- Jisajili kwenye mfumo wa mbolea (FIS)
- Tumia kiunganishi cha FIS: fis.tfra.go.tz kuomba leseni
- Jaza taarifa muhimu
- Toa taarifa zote zinazohitajika kwa ajili ya maombi ya leseni ya Kampuni au Mtu Binafsi
- Chagua “Usajili kwa Muuzaji wa Mbolea”
- Bonyeza chaguo hili kuanza mchakato wa maombi
- Ukurasa mpya utafunguka
- Jaza maelezo yote yanayohitajika kwenye ukurasa huu
- Jaza taarifa kwa usahihi
- Jina la biashara lililosajiliwa: Andika kama lilivyo kwenye Cheti cha Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)
- Jina la mtaalamu aliyepata mafunzo: Andika kama lilivyo kwenye cheti cha mafunzo
- Ambatanisha nyaraka muhimu
- Cheti cha Nambari ya Utambulisho wa Kodi (TIN)
- Cheti cha Usajili wa Kampuni (ikiwa ni Kampuni)
- Cheti cha Mafunzo ya Mbolea
- Namba ya NIDA(endapo sio kampuni)
- Wasilisha maombi
- Mamlaka itapokea maombi yako kwa ajili ya tathmini na uchakataji
- Tathmini ya maombi
- TFRA itapitia taarifa na nyaraka zilizowekwa
- Ikiwa maombi yako yatakidhi masharti, leseni itatolewa
- Ikiwa kuna makosa au taarifa zisizo sahihi, maombi yatakataliwa na mwombaji ataarifiwa kupitia akaunti yake ili kufanya marekebisho
- Chapisha leseni
- Baada ya maombi kuthibitishwa, mwombaji atachapisha leseni kupitia akaunti yake, tayari kwa matumizi
Kumbuka: Viambatanisho vyote lazima viwe katika mfumo wa PDF.
