USAJILI WA MBOLEA
Usajili wa Mbolea ni mchakato rasmi wa kisheria wa kusajili mbolea ili iruhusiwe kuingizwa, kuzalishwa, kusambazwa na kutumika nchini. Lengo lake ni kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa mbolea kwa mazao na mazingira.
Mambo Muhimu katika Usajili wa Mbolea
-
Maombi ya Usajili
Muombaji huwasilisha taarifa za mbolea kupitia mfumo wa mbolea FIS (aina, muundo wa virutubisho, matumizi yaliyokusudiwa). -
Nyaraka za Kuambatisha
-
Cheti cha uchambuzi
-
Taarifa za usalama wa mbolea
-
Kibandiko
-
-
Uchambuzi wa Maabara
Mbolea hupimwa ili kuthibitisha viwango vya virutubisho na usalama. -
Majaribio ya Shambani (ikiwa yanahitajika)
Hutathmini ufanisi wa mbolea kwa mazao husika. -
Uhakiki na Uidhinishaji
Mamlaka husika hukagua nyaraka na matokeo kabla ya kutoa kibali. -
Kutoa Cheti cha Usajili
Mbolea ikikidhi vigezo, husajiliwa na kupewa cheti.
