Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akizungumza na wadau walioshiriki kwenye warsha ya kupokea taarifa ya utafiti uliofanywa na IFDC kuhusu uwezekano wa kuwekeza kwenye viwanda vya mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini. Warsha imefanyika katika hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam tarehe 12/11/2024
Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji wa Ndani na Ununuzi wa Mbolea kwa pamoja, Louis Kasera akifuatilia taarifa ya utafiti wa uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini katika warsha iliyofanyika katika hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni Kaimu Meneja wa Huduma za Sheria, Fikiri Mboya
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti, Elizabeth Bolle (mwenye suti nyeusi) akifuatilia taarifa ya utafiti wa uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini katika warsha iliyofanyika katika hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni Kaimu Meneja wa Huduma za Sheria, Fikiri Mboya
Wadau wa tasnia ya mbolea wakifuatilia wasilisho lililotolewa kufuatia utafiti uliofanywa na IFDC kuhusiana na uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea kunakotokana na malighafi zinazopatikana nchini kama vile makaa ya mawe, gesi asilia, phosphate na mengineyo
Watafiti kutoka IFDC wakifuatilia mada wakati wa warsha iliyolenga kupokea taarifa na maoni ya utafiti uliofanyika kubainisha fursa zilizopo za uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea kwa kutumia rasilimali zinazopatikana nchini . Warsha imefanyika tarehe 12 Novemba, 2024 katika hoteli ya protea Jijini Dar Es Salaam