Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
VIBALI
VIBALI

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) hutoa huduma za utoaji wa vibali vya kuingiza na kutoa mbolea nchini kwa mujibu wa Sheria ya Mbolea Na. 9 ya mwaka 2009. Lengo la huduma hizi ni kuhakikisha nchi inakuwa na mbolea za kutosha, salama na zenye ubora unaokubalika kwa ajili ya kuendeleza kilimo endelevu.

Ili kuhakikisha mbolea inayoingia nchini inakidhi viwango vya ubora, Mamlaka humtaka mfanyabiashara kuwasilisha nyaraka zenye taarifa muhimu zinazothibitisha ubora na uhalali wa mzigo husika.

Maombi ya vibali vya kuingiza na kutoa mbolea nchini hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Taarifa za Mbolea FIS.


Kibali cha Kuingiza Mbolea Nchini

Ili kupata kibali cha kuingiza mbolea nchini, mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuambatisha nyaraka zifuatazo:

  • Hati ya madai/malipo (Commercial Invoice) inayoonesha thamani ya mzigo ikiwa ni pamoja na FOB, Insurance na Freight

  • Cheti cha Uchambuzi (Certificate of Analysis)

  • Hati ya mzigo (Bill of Lading / Airway Bill / Packing List)

Mwombaji atalazimika kulipa ada ya kibali cha kuingiza mbolea inayolingana na asilimia 1.5 ya thamani ya CIF ya mzigo ili kibali kitolewe.


Kibali cha Kutoa Mbolea Nje ya Nchi

Ili kupata kibali cha kutoa mbolea nje ya nchi, mwombaji atajaza fomu ya maombi na kuambatisha hati ya madai/malipo (Commercial Invoice).

Mwombaji atalipa ada ya kibali cha kutoa mbolea nje ya nchi kiasi cha Dola za Marekani 0.5 kwa kila tani moja ya mbolea.