Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ruzuku ya mbolea inatolewa kwa wakulima wa mazao yote.
Nyaraka zinazotakiwa wakati wa usajili ni
1. Kitambulisho cha Taifa au Kitambulisho cha mpiga kura
2. Simu ya mkononi kwa ajili ya kupokea ujumbe wa uthibitisho (SMS) unaoonyesha namba ya mkulima.
3. Taarifa za shamba kama eneo la shamba, aina ya zao analolima na mahali lilipo shamba.
4....
Mkulima anaweza kujisajili kwenye mpango wa ruzuku ya mbolea kupitia Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Afisa ugani wa Kijiji au kata.
Mbolea zote za kupandia na kukuzia zipo kwenye mpango wa ruzuku ya mbolea.
Ili kupata ruzuku ya mbolea mkulima lazima awe amejisajili rasmi kwenye mpango wa ruzuku ya mbolea unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na kupata namba ya mkulima.
A: Majibu hutolewa ndani ya siku tatu (3) za kazi.
Kipimo
Gharama (Tsh)
Kiwango cha Nitrojeni (N-NO3, N-NH4)
110,000
Kiwango cha Foriforasi
110,000
Kiwango cha virutubisho (Na, K, Ca & Mg)
110,000
Kiwango cha mboji
110,000...
A: Wanaoweza kupeleka sampuli ni:
- Waingizaji wa mbolea
- Wafanyabiashara wa mbolea
- Taasisi za utafiti na elimu
- Wakulima na watu binafsi
- Wazalishaji wa ndani
- TFRA kwa ajili ya ufuatiliaji na udhibiti
A: Maabara ya Taifa ya Mbolea inapima viwango vya virutubisho vilivyomo kwenye sampuli za mbolea, visaidi vyake pamoja na afya ya udongo ili kuhakikisha ubora na ufanisi wake.
A: Ndiyo, yanatolewa bure na TFRA.
