Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
TFRA, Wazalishaji wa mbolea waazimia utoshelevu wa mbolea nchini ifikapo 2030
21 Mar, 2024 09:00AM-13:30PM
TFRA
PR

Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA), imekutana na kufanya mazungumzo na wazalishaji wa mbolea nchini ambapo wamejadili mustakabali wa tasnia ya mbolea wenye lengo la kupunguza uingizaji wa mbolea ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka, Joel Laurent wakati wa kikao baina ya TFRA na wazalishaji wa ndani wa mbolea kilichofanyika tarehe 20 Machi, 2024 katika ukumbi wa Mamlaka jijini Dar Es Salaam

Amesema kupungua kwa utegemezi wa mbolea kutoka nje ya nchini kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni na hivyo kuongeza mchango wa Sekta ya Kilimo kwenye Uchumi wa Taifa na kufikia asilimia 10.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho Mkurugenzi Laurent amesema, maono ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ifikapo 2030 ni kuhakikisha nchi inajitegemea kwa asilimia 100 katika kupata pembejeo ya mbolea kwa kutumia viwanda vya ndani.

Ameeleza kuwa ili kufikia azima hiyo, Mamlaka imekutana na wazalishaji wa ndani ili kujadiliana maeneo ya kufanyia kazi ili kuwawezesha kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kutakakopelekea kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo na hivyo nchi kujitosheleza.

Laurent amebainisha kuwa, Ili kufikia ajenda 10/30: Kilimo ni Biashara, juhudi zinafanyika ili kuongeza kiasi cha mbolea inayotumika kwenye hekta 1 kutoka kg. 19 mpaka wastani wa kilo 50 kwa hekta moja.

Amesema wastani wa mahitaji ya mbolea kwa mwaka ni takribni tani 848,000 kwa mbolea zote na kueleza kuwa matarajio ya Mamlaka ni kuongezeka kwa matumizi ya mbolea ifikapo 2030 kutakako tokana na uelewa wa manufaa ya kutumia mbolea kwenye kilimo, uzingatiaji wa kanuni bora za kilimo kama zinavyoelekezwa na Maafisa Ugani wetu kayika maeneo yao, wakulima kuhamasishwa kutumia mbolea zinazozalishwa nchini pamoja na bei ya bidhaa hiyo kuwa himilivu kutakakopelekea kila mkulima kumudu gharama hizo.

Kwa upande wake, Tosky Hans Mkurugenzi Mtendaji wa Minjingu Mining and fertilizer, ameipongeza Mamlaka kwa kuitisha kikao kilichoangazia namna tasnia ya mbolea nchini inavyoweza kuongeza uzalishaji na utoshelevu kulingana na mahitaji ya nchi.

TFRA, Wazalishaji wa mbolea waazimia utoshelevu wa mbolea nchini ifikapo 2030