FERTILIZER SUSBSIDY PROGRAM 2022-2023
Katika msimu wa 2022/2023, Serikali imepanga kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa lengo la kupunguza gharama ya mbolea kwa mkulima ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani. Utoaji wa ruzuku utazingatia mahitaji halisi ya mkulima kulingana na taarifa za usajili na bajeti ya Serikali iliyotengwa.
Mbolea zitakazohusika kwenye ruzuku ni mbolea za kupandia na kukuzia ambapo DAP kwa ajili ya kupandia na Urea kwa ajili ya kukuzia ambazo ni takribani 50% ya matumizi ya mbolea nchini. Mbolea za kupandia na kukuzia za aina zingine zitahusika kwenye ruzuku kulingana na mahitaji ya soko. Aidha, ili kuhamasisha matumizi ya mbolea zinazozalishwa nchini, mbolea zinazozalishwa na viwanda vya ndani zitaingia kwenye mpango wa ruzuku kulingana na mahitaji ya soko.
Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority-TFRA) itatumia mfumo wa kielektroniki katika kutoa ruzuku ya mbolea kwa lengo la kuongeza kuongeza ufanisi wa utoaji wa ruzuku, kupunguza mianya ya udanganyifu na gharama za usimamizi. Mfumo huo utatumia programu maalum ya kidigitali kusajili wakulima, wasambazaji/wazalishaji, mawakala pamoja na kuratibu usambazaji wa mbolea kwa wakulima na malipo ya mbolea ya ruzuku.
Utekelezaji wa mpango wa ruzuku ya mbolea utahusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Sekeretariti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Waingizaji/Wazalishaji wa Mbolea, Mawakala (Agrodealers) wa Mbolea, Taasisi za Fedha, Wakulima na wadau wengine muhimu.
Mwongozo huu umeandaliwa kwa lengo la kutoa maelekezo ya utaratibu wa utoaji na usimamizi wa ruzuku ya mbolea ikiwa ni pamoja na kuainisha ngazi za utekelezaji na wajibu wa kila wadau katika usimamizi wa ruzuku ya mbolea kwa msimu wa 2022/2023.
Mwongozo wa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea Mwaka 2022-2023
Mwongozo wa mpango wa ruzuku ya mbolea ya mwaka 20222023
Orodha ya Kwanza ya Mawakala Waliosajiliwa Kusambaza Mbolea ya Ruzuku 2022/23
Orodha ya mawakala waliosajiliwa kuuza na kusambaza mbolea za ruzuku 2022 2023