Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Watumishi wa umma waaswa kutofanya kazi kwa mazoea
29 May, 2024
Watumishi wa umma waaswa kutofanya kazi kwa mazoea

Imeelezwa kuwa, utendaji kazi wa mazoea unaofanywa na watumishi wa umma unasababishwa na kutokuwajibishwa kwa kutokuwa na matokeo katika nafasi zao.Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ndani ya mkoa wa Ruvuma.Akihoji kwa mifano, viongozi wa ngazi mbalimbali aliokutana nao wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Songea na kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru , Dkt. Diallo alitaka kujua endapo kuna kiongozi yeyote aliyeomba kupewa taarifa ya upimaji wa afya ya udongo kwa maafisa ugani waliokabidhiwa vifaa vya kupima na kubaini afya ya udongo katika maeneo yao.Aidha, alihoji endapo yupo kiongozi yeyote katika ngazi ya Mkoa au Wilaya aliyechukua hatua ya kuhakiki taarifa za usajili zilizotolewa na wakulima kwa ajili ya kunufaika na mbolea ya ruzuku?Mara baada ya kubaini mambo hayo kutokufanyika Dkt. Diallo aliwashauri viongozi hao kufanya hivyo na kuwawezesha maafisa wao kuhakiki taarifa za wakulima ili mbolea inayotolewa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inawanufaisha watanzania na si vinginevyo.Aidha, Dkt. Diallo ameshauri kuwa, kutokana na hali ya kuwa na mvua nyingi katika Mkoa wa Ruvuma, ni dhahiri eneo hilo linaadhiriwa na hali ya mmomonyoko wa udongo na kushauri wakulima kulima kilimo cha kontua na pia kupima afya ya udongo mara kwa mara ili kujua hali ya udongo wao.Akizungumza kwa niaba ya kampuni za mbolea mkoani Ruvuma, Ayubu Njogela, amesema kampuni za mbolea zimejipanga kuhakikisha mbolea zinafikishwa kila mahala na kwa wakati.Ameishukuru Mamlaka kwa kuhakikisha mawakala na vyama vya ushirika vimesajiliwa na kupata namba za uwakala na kuwaeleza wakulima kuwa mbolea zipo na zitasambazwa kulingana na mahitaji na bei zitauzwa kulingana na umbali.Akifunga kikao hicho, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Jumanne Mwankoh amekiri kupokea maoni na ushauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA na kuahidi kufanyia kazi.