Wakulima washauriwa kununua mbolea kwa pamoja

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kupitia vyama vya ushirika inawahamasisha wakulima nchini kununua mbolea kwa pamoja kutoka kwa wazalishaji/makampuni yanayoingiza mbolea moja kwa moja badala ya mkulima mmoja mmoja kununua kutoka kwa wafanyabiashara wa kati ili kununua mbolea hiyo kwa bei ya jumlana hivyo kuipata kwa bei nafuu tofauti na kila mkulima akinunua kiasi kidogo cha mbolea.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ndani na ununuzi wa Mbolea wa Pamoja, Joseph Charos alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki.
Charos alieleza kuwa, Kutokana na bei za mbolea katika soko la dunia kuendelea kupanda, bei za soko la ndani pia zimeendelea kuongezeka. Alisema, kwa mfano, wastani wa bei ya mkulima (Retail price) kwa mbolea ya Urea umepanda kutoka Sh.53,318mweziDesemba, 2020 na kufikia Sh. 104,069 mweziDesemba, 2021kwa mfuko wa kilo 50, wakati wastani wa bei ya mbolea ya DAP umepanda kutoka Sh.66,995mweziDesemba, 2020hadi Sh. 109,179 mweziDesemba, 2021kwa mfuko wa kilo 50 sawa na ongezeko la95% na63% mtawalia.
Alifafanua kuwa, kwa mujibu wa bei za mbolea zilizokuwa zikitangazwa na soko la dunia katikakipindi cha Julai - Desemba 2021, kwa wastani bei za mbolea zilizoingia nchini zilikuwa nafuu ambapo kwa mbolea ya UREA, bei ya chanzo (FOB) katika soko la dunia kwa mwezi Julaihadi Desembailikuwa kati ya dola za marekani420 hadi 1,000kwa tani wakati wastani wa bei hadi hapa nchini (CIF Value) kwa mbolea iliyoingiakatika kipindi hichonikati yadola za marekani570 hadi 1,398kwa tani.
Akielezea kwa upande wa DAP, Charos alisema bei ya chanzo (FOB) katika soko la dunia kwa mwezi Julaihadi Desembailikuwa kati ya dola za marekani550hadi 912 kwa tani wakati wastani wa bei hadi hapa nchini (CIF Value) kwa mbolea iliyoingianchini katika kipindi hichonikati yadola za marekani659 hadi 810kwa tani.
Kufuatia bei za mbolea kuwa juu kwenye soko la dunia, soko la ushindani nchini limesababisha wafanyabiashara wafanye jitihada za kutafuta mbolea kutoka kwenye vyanzo vyenye bei nafuu ili kupunguza bei ya mbolea kwa wateja wao.
Akihitimisha taarifa yake Charos alisema, Kwa ujumla, bei za mbolea zilizoingianchinikatika kipindicha Julai- Desemba 2021zimepanda kwa mboleazotezikilinganishwa na bei za kipindi kama hiki mwaka 2020/2021.
Aliongezakuwa, wastani wa bei ya kufikishia mbolea ya DAP hapa nchini (CIF) kwa mwezi Desemba, 2020 ilikuwa dola za kimarekani 362 ikilinganishwa na wastani wa dola za kimarekani 810 kwa mbolea iliyoingia mwezi Desemba, 2021 sawa na ongezeko la 123%, ambapo kwa mbolea ya Urea, bei ya kuifikisha hapa nchini (CIF) kwa mwezi Desemba, 2020 ilikuwa dola za marekani 310 wakati bei ya mbolea iliyoingia chini mwezi Desemba, 2021 ni dola za marekani 1,398 sawa na ongezeko la 350%.
Hata hivyo, mamlaka inaendelea na juhudi za kuwahamasisha wakulima kupitia vyama vya ushirika na wataalam wa kilimo, kutumia mbolea mbadala katika shughuli za kilimo zinazopatikana kwa gharama nafuu na kuwataka kuzingatia ushauri wa wataalam.