Wakulima jitokezeni kujisajili/kuhuisha taarifa zenu- Silinde

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (Mb) amewataka wakulima ambao hawajajisajili kwenye mfumo wa kigitali wa wakulima kuhakikisha wanajisajili ili wapate mbolea ya ruzuku inayotolewa na serikali.
Mhe. Silinde ameyasema hayo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Chipukizi manispaa ya Tabora mkoani Tabora.
Naibu Waziri Silinde ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima ambao wameshasajiliwa wafike kwenye ofisi za watendaji wa vijiji wakahuishe taarifa zao.
Aidha Mhe. Silinde ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuendelea na maboresho ya mfumo wa mbolea za ruzuku mawakala waendelee kutoa huduma ili wakulima wapate mbolea kwa wakati na kwa utaratibu rahisi.
Naibu Waziri Silinde, ameisisitiza TFRA kushirikiana kwa karibu na Mamlaka za Serikali za Mitaa vituo vyote vya kusamba mbolea vinakuwa na mawakala au vyama vya msingi vya ushirika ili wakulima wasifute mbolea umbali mrefu.
Awali akitoa salamu za mkoa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ameishukuru Wizara ya Kilimo kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Mkoa wa Tabora.
Aidha, Dkt. Buriani amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa miradi ya skimu za umwagiliaji mkoani Tabora yenye thamani ya Shilingi Bilioni 57.
Ameongeza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwekaji wa miundombinu ya umwagiliaji wenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 kwenye shamba la kuzalishia mbegu la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) wilayani Nzega mkoani Tabora.
Kwu pande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ,Bw. Joel Laurent mesema maboresho yanayoendelea kufanywa yataendelea kuongeza matumizi ya mbolea kwa wakulima.
Amefafanua kuwa katika msimu wa mwaka 2023/2924 matokeo ya matumizi ya mbolea katika mpango wa ruzuku ya yanatarajiwa kufikia tani 430,000 sawa na ongezeko la asilimia 12 ukilinganisha na msimu wa 2022/23.