TFRA na uhamasishaji matumizi sahihi ya mbolea
29 May, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DKt. Stephan Ngailo amewasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kuzungumza na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Lindi, Majid Myao.
Akieleza lengo la ziara hiyo, Dkt. Ngailo amesema katika kuelekea katika kuadhimisha siku ya mkulima ya mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea yenye lengo la kuwahamasisha wakulima kutumia mbolea bora katika shughuli zao za kilimo ili kuongeza tija na kipato katika kazi zao.
Amesema, lengo kubwa ni kujua jinsi gani tutaweza kuifikia siku hiyo kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kugawana majukumu baina ya serikali ya mkoa na Mamlaka.