TFRA kanda ya Kaskazini wapongezwa kwa utendaji mzuri

Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony M. Diallo amewapongeza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya.
"Mnafanya kazi kubwa sana kwa idadi yenu huwezi kufikiri kuwa ndio mnaotekeleza majukumu haya mazito" Aliongeza Diallo.
Pongezi hizo amezitoa tarehe 14 Machi, 2023 alipoanza ziara yake ya siku mbili katika kanda hiyo ikiwa na lengo la kujifunza juu ya utendaji kazi wa viwanda vinavyozalisha mbolea pamoja na kuendelea kujifunza masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo kwa vitendo.
Akizungumza na watumishi hao katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za kanda hiyo, Dkt. Diallo alieleza nia ya kuendelea kuboresha na kuimarisha mifumo inayosimamia Mamlaka ili kupunguza mianya ya upotevu wa fedha za Serikali.
Dkt. Diallo aliongeza kuwa, pamoja na kujifunza kutoka kwa wazalishaji wa mbolea yeye pia ni mbobevu katika eneo hilo na kueleza amejikita katika sekta ya viwanda kwa muda mrefu.
Akiwasilisha taarifa ya Kanda, Kaimu Meneja wa TFRA Sheila Mrogoro alisema, Kanda ya Kaskazini inasimamia mikoa 4 ikiwa ni (Mkoa wa) Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga.
Sheila alieleza kwa kifupi majukumu yaliyotekelezwa na Ofisi yake kwa Mwaka wa fedha 2022- 2023 kuwa ni pamoja na; ukaguzi wa wafanyabiashara na wazalishaji wa mbolea, ukaguzi wa nguzo (premises) za kuzalishia na kuhifadhia mbolea, kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wafanyabiashara wa mbolea ili kufikisha utaalamu huo kwa wateja wao(wakulima) na nyingine zilizomo ndani ya mamlaka yao