TFRA yapongezwa upatikanaji wa mbolea Arumeru

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Kaganda ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kuhakikisha mbolea ya ruzuku inapatikana katika Wilaya hiyo.
Kaganda amesema, upatikanaji wa mbolea kwa wakati unawawezesha wakulima kuhudumia mashamba yao kwa kutumia mbolea stahiki kwa wakati, na hivyo kuongeza uzalishaji utakaokuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.
Mhe. Kaganda ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Mamlaka kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa Mkutano wa mwaka wa wadau wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuwatilifu Tanzania ( TPHPA) uliofanyika tarehe 21 June, 2024 katika Viunga vya ofisi ya Mamlaka hiyo Jijini Arusha.
Kaganda ameeleza kuwa kwa sasa mbolea inapatikana na malalamiko yamepungua kwa kiasi kukubwa ukilinganisha na msimu wa kilimo uliopita.
Mkutano huo umefanyika sambamba na Maonesho ambayo TFRA pia imeshiriki.