Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Tani 9,361.48 za mbolea za ruzuku kuwanufaisha wakulima Kilimanjaro
29 May, 2024
Tani 9,361.48 za mbolea za ruzuku kuwanufaisha wakulima Kilimanjaro

Zaidi ya Shilingi bilioni 17 zimetolewa na serikali ili kugharamia ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa Kanda ya Kaskazini mwa Tanzania kuanzia mwezi Agosti 2022 hadi sasa na kuwanufaisha wakulima wa mazao ya kibiashara, chakula ikiwa ni pamoja na mazao ya mbogamboga na matunda.

Kiasi cha tani 9,361 zambolea zimewafikia wakulima na kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na tijakayika kilimo, kuimarisha shughuli za kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Kaskazini, Gothard Liampawe alipokuwa akizungumza na wanahabari waliopiga kambi katika kanda anayoisimamia kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa mpango wa ruzuku za mbolea unaotekelezwa na Seriikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa msimu wa kilimo 2022/2023.

Liampawe amesema ruzuku hiyo itawanufaisha wakulima 1,309,199 wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga pindi usajili utakapokamilika na kubainisha mkoa wa Kilimanjaro umeongoza kwa kusajili wakulima158,399 kwenye mfumo wa kidijitali baada ya daftari 2160 za kusajili wakulima kusambazwa kwenye vijiji vya mkoa huo na kufikia malengo kwa asilimia 39.