Ongezeko matumizi ya mbolea kudhihirisha tija shughuli za kilimo- Dkt. Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa,ongezeko la kiasi cha mbolea inayotumika kwenye shughuli za kilimo ni ishara tosha kuwa kilimo kinaleta tija kwa wakulima.
Amesema, kuongezeka kwa uzalishaji kwenye miradi mbalimbali ya kilimo inayosimamiwa na vijana kupitia mradi wa Kuijenga Kesho iliyo Bora (BBT) chini ya Wizara ya Kilimo ni kipimo cha matumizi mazuri ya mbolea.
Amebainisha hay oleo tarehe 07 Agosti, 2023 alipokuwa akizungumza na vijana barani Afrika juu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali mbalimbali katika kuhakikisha vijana wanaingia kwenye shughuli za uzalishaji na kupunguza changamoto ya ajira inayowakabili.
Ameeleza ishara nyingine kuwa ni kuongezeka kwa mchango kwenye uchumi utokanao na kilimo, kiasi cha mazao yanayopelekwa sokoni Pamoja na kushuka kwa gharama za chakula sokoni.
Mjadala huu ni mwendelezo wa mijadala mbalimbali iliyofanyika kuanzia tarehe 5 - 8 Agosti, 2023 ambapo zaidi ya washiriki 4000 kutoka nchi mbalimbali Afrika wameshiriki mkutano huo wa Kimataifa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika