Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
MATUMIZI YA MBOLEA NCHINI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 60
04 Nov, 2026
MATUMIZI YA MBOLEA NCHINI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 60

MATUMIZI YA MBOLEA NCHINI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 60

Na. Mwandishi wetu, GAIRO, MOROGORO
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema matumizi ya mbolea nchini yameongezeka na kufikia tani 1,132,799 katika msimu wa 2025/2026, kutoka tani 580,628 zilizotumika wakati mpango wa ruzuku ulipozinduliwa msimu wa 2022/2023.

Ameyasema hayo leo Novemba 1, 2026, wakati akitoa hotuba yake katika Kongamano la Siku ya Mbolea lililofanyika sambamba na Maonesho ya Tano ya Gairo Kilimo Biashara Expo mkoani Morogoro, ambapo alibainisha kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 60.

Akizungumzia hali ya Mkoa wa Morogoro, alieleza kuwa katika Wilaya ya Gairo matumizi ya mbolea yameongezeka kwa asilimia 26.4 kutoka tani 221.8 msimu wa 2022/2023 hadi kufikia tani 839.35 katika msimu wa 2025/2026, ishara inayodhihirisha mwitikio chanya wa wakulima katika kilimo cha kisasa.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala Wilaya ya Gairo, Jeremiah Mapogo amepongeza mamlaka kuwa sehemu ya udhamini mkuu katika maonesho ya Tano ya Kilimo Biashara na akaomba juhudi za kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya mbolea, kuchagua mbolea kulingana na mahitaji ya mazao ili kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo unakuwa endelevu.

Kwa upande wake, mkulima Lameck Msigala ameipongeza TFRA kwa kuwafikishia elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kupitia maonesho hayo, sambamba na kuwasajili katika mfumo wa Ruzuku ya Mbolea, hatua itakayowawezesha kunufaika na mpango huo na kurahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu.