TAARIFA KWA UMMA KUTOA MAONI KUHUSU MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA KANUNI ZAMBOLEA ZA MWAKA 2026
TAARIFA KWA UMMA
MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA MBOLEA ZA MWAKA 2026 NA KANUNI ZA MBOLEA (UFIFILISHAJI MAKOSA) ZA MWAKA 2026
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority – TFRA) inautangazia umma na wadau wote tasnia ya mbolea nchini kuwa inafanya mapitio ya Kanuni za Mbolea za Mwaka 2026 pamoja na Kanuni za Mbolea (Ufifilishaji Makosa) za Mwaka 2026.
Katika kuimarisha ushirikishwaji wa wadau na kuhakikisha kuwa mapendekezo ya marekebisho hayo yanazingatia mahitaji ya sekta ya mbolea nchini, TFRA inawaalika wadau wote kuwasilisha maoni na mapendekezo yao kuhusu marekebisho hayo ili yazingatiwe kabla ya kuwasilishwa katika hatua zinazofuata za kisheria.
Wadau wanahimizwa kuwasilisha maoni na mapendekezo kwa maandishi mnamo au kabla ya tarehe 28 Oktoba, 2026 kupitia njia zifuatazo:
Kwa njia ya posta: Mkurugenzi Mtendaji, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA),
S.L.P. 46236, Dar es Salaam.
Kwa njia ya barua pepe: info@tfra.go.tz
Nakala za mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za Mbolea za Mwaka 2026 pamoja na Kanuni za Mbolea (Ufifilishaji Makosa) za Mwaka 2026 zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya TFRA.
TFRA inawahimiza wadau wote kutumia fursa hii kushiriki kikamilifu katika mchakato wa mapitio ya kanuni hizo kwa kutoa maoni na mapendekezo yatakayochangia kuboresha mfumo wa usimamizi na udhibiti wa tasnia ya mbolea nchini na kuendeleza sekta ya kilimo kwa ujumla.
Imetolewa na :
MKURUGENZI MTENDAJI
23 Oktoba, 2026
