Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Matamanio ya Rais Samia yafikiwa kiwanda cha mbolea ITRACOM
29 May, 2024
Matamanio ya Rais Samia yafikiwa kiwanda cha mbolea ITRACOM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa amesema matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwa na kiwanda kikubwa cha mbolea nchini yamefikika baada ya mwekezaji wa kiwanda cha Itracom kuanza uzalishaji.

Amesema kiwanda cha mbolea cha itracom ambacho kinauwezo wa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka ambapo kwa sasa mitambo iliyoanza kuzalisha ni tani 200,000. Pia kiwanda hiki cha mbolea kitaambatana na viwanda vingine vidogo vidogo ikiwa ni pamoja na kiwanda cha kuzalisha Chokaa Mazao (Agricultural lime), kiwanda cha kutengeneza mifuko, kiwanda cha kusindika maziwa na cha kuchakata samadi inayotumika kama malighafi wakati wa utengenezaji wa mbolea.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana tar 20 Desemba, 2022 alipotembelea kiwanda hicho kilichojengwa katika eneo la Nala Jijini Dodoma ili kujionea hatua iliyofikia na kukagua shughuli zinazoendelea kiwandani hapo.

Majaliwa amekiri kuwa ahadi ya mwekezaji ya kuanza uzalishaji mwezi wa 8/9, 2022 imetimia kwani tayari uzalishaji umeanza na wakulima watanunua mbolea hizo kwa bei ya ruzuku.

Amesema uwepo wa kiwanda hicho unawahakikishia watanzania upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu, uwepo wa ajira kwa zaidi ya watu 5000, kutaongeza mchango wa kikodi utakaongizwa kwenye utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya wananchi wa eneo husika na Tanzania kwa ujumla.