Kiongozi wa mbio za Mwenge 2026 aipa heko TFRA Kwa kuwashika mkono vijana
Kiongozi wa mbio za Mwenge 2026 aipa heko TFRA Kwa kuwashika mkono vijana
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2026, Wazo Mwang'onda ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kuwasaidia vijana zaidi ya 160 kwa kuwapatia mbolea ambayo imewaletea tija shambani, huku akiomba waendelea kuwasaidia zaidi kwa kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo hiyo muhimu ili wafanye kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi.
Mwang'onda ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua banda la TFRA katika eneo la mkesha wa mwenge wilayani makete, na kuwasihi wataalamu kutoka Mamlaka hiyo kujikita zaidi kuwasaidia vijana ili waweze kuinuka kichumi.
Aidha,ameeleza kuwa vijana ndio nguvu kazi pekee inayoweza kuleta mabadiliko nchini kupitia sekta ya kilimo iwapo watapewa elimu sahihi ya kufanya kilimo chenye tija ambacho kitaleta matokeo ya wazi.
Naye Afisa Udhibiti Ubora TFRA Nyanda za Juu Kusini, Chrisantus Funda amesema Mamlaka itaendelea kuwasaidia vijana kwa kutoa elimu stahiki na kuwasogeza karibu kwa uangalizi kupitia maafisa kilimo wa wilaya ili wengi wajikite katika sekta ya kilimo itakayowasaidia kuinuka kichumi na kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira nchini.
"Ikumbukwe kwamba TFRA imekuwa sehemu ya kuwasaidia vijana katika sekta ya kilimo baada ya kutoa mifuko zaidi ya 200 ya mbolea kupitia programu iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Kissa Kasongwa ambayo inewanufaisha vijana wengi.
Aidha, Funda amemshukuru kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Wazo Michael Mwang'onda kwa kutambua juhudi za TFRA kwa kuendelea kuwa karibu na wakulima hususani maeneo ya vijijini na kusimamia upatikanaji wa mbolea.
