Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Yakiendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam
09 Jul, 2024
Maonesho ya kimataifa ya biashara yanaendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wanaendelea kutoa huduma mbalimbali katika banda lao lililopo chini ya wizara ya Kilimo katika hema la Katavi. Wageni kutoka taasisi na mataifa mbalimbali wanaendelea kupata elimu na taarifa za huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo.