Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Imarisheni Udhibiti wa Mbolea Mipakani - Silinde
29 May, 2024
Imarisheni Udhibiti wa Mbolea Mipakani - Silinde

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Ernest Silinde ameitaka Bodi ya wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuongeza kasi ya udhibiti wa mbolea hususan katika maeneo ya mipakani ili mbolea ya ruzuku inayotolewa na serikali iwanufaishe watanzania na si kutoroshwa nje ya nchi.



Silinde ameyasema hayo leo tarehe 30 Septemba, 2023 alipotembelea na kuzungumza na uongozi wa Mamlaka hiyo katika ziara iliyolenga kujifunza namna Mamaka inavyofanya kazi na kutoa maelekezo ya Serikali katika kuimarisha utendaji kwa maslahi mapana ya taifa.



Amesema awali kilimo kilikuwa hakieleweki lakini kutokana na Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuamua kuweka nguvu kubwa katika kuinua Sekta ya Kilimo wakulima wameelewa na wameanza kufuatilia na kutokana na hilo changamoto mbalimbali zinaibuliwa kutoka ngazi za chini.



Aidha, Mhe. Silinde ameitaka TFRA kuanza zoezi la usambazaji wa mbolea mapema ili kupunguza malalamiko ya kuwafikishia wakulima mbolea kwa kuchelewa kama ilivyojitokeza msimu uliopita wa kilimo.



Amesema mbolea zikipelekwa mapema itawawezesha wakulima kujiandaa mapema kwa kununua na kuhifadhi mbolea majumbani mwao wakisubiri msimu wa kupanda.



“Mbolea iliyopo sasa ianze kusambazwa isisubiri Wakatip wa msimu ndipo tuanze kukimbizana kupeleka mbolea kwa wakulima” Mhe. Silinde alisisitiza.



Katika kuhakikisha ruzuku ya mbolea inayotolewa na serikali inawafikia walengwa, Naibu Waziri Silinde ameitaka TFRA kufanya uhakiki wa taarifa za usajili wa wakulima ilikuondoa changamoto za mawakala kuuza mbolea kwa wakulima waliotoa taarifa za uongo wakati wa usajili.



Ameipongeza Mamlaka kwa kuja na mfumo wa ramani unaoiwezesha kuoa maeneo walipo mawakala, kiasi cha mbolea walichonacho mawakala wa mbolea kwa nchi nzima na kueleza hiyo itasaidia kufuatilia upatikanaji wa mbolea kwa wakati katika maeneo yote



Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku, Louis Kasera amesema utoajiwa mbolea ya ruzuku kwa wakulima kumeamsha hari ya wakulima wengi kutumia mbolea katika kilimo chao na hivyo uhitaji wa bidhaa hiyo kuwa mkubwa.



Amesema mamlaka imetatua changamoto ya usambazaji iliyojitokeza msimu uliopita wa kilimo kwa kusajili vyama va ushirika 198 nchi nzima na Vyama vidogo vya ushirika (AMCOSS) zaidi ya 2000 vitakavyosaidia kufikisha mbolea kwa wakulima wao hata katika maeneo ya pembezoni.



Amesema, lengo la Mamlaka mkulima asitembee zaidi ya umbali wa kilomita 15 kwenda kutafuta mbolea na hivyo wamepanga bei elekezi kulingana nae neo ambalo mbolea inafika.



Katika kuongeza Udhibiti wa kuuza mbolea mara mbili, Louis amesema Mamlaka imeboresha mfumo ambapo kila mfuko wa mbolea utakaouzwa namba ya siri itakayokuwa imetumika haitatumika tena na mkulima atapokea namba nyingine itakayomruhusu kununua mbolea kulingana na ukubwa wa shamba alioandikisha wakati wa usajili.



Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (DCS), Victoria Elangwa alishukuru uamuzi wa Naibu Waziri Silinde kutembelea Mamlaka na kueleza kuwa ujio wake utachochea ari ya kufanya kazi kwa menejimenti na watumishi wa Mamlaka.