Dkt. Nchemba Aipongeza TFRA kwa Mchango Wake katika Kukuza Sekta ya Kilimo
Dkt. Nchemba Aipongeza TFRA kwa Mchango Wake katika Kukuza Sekta ya Kilimo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza na kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuendelea kufanya kazi kwa bidii, akieleza kuwa mamlaka hiyo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo tarehe 19 Mei 2026, alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma, ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB).
Aidha, Dkt. Nchemba amewataka wananchi kuacha kufanya biashara kwa njia holela na kuhakikisha wanatumia mifumo iliyorasimishwa na serikali ili kuongeza tija katika uzalishaji wao.
Pamoja na hayo, amezitaka taasisi mbalimbali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za kutumia mifumo iliyorasimishwa, akieleza kuwa mifumo hiyo ni jawabu la kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo utapeli na hasara zinazotokana na uuzaji holela wa mazao na pembejeo za kilimo.
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu katika banda la Mkoa wa Singida, Issack Charles ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mpango wa ruzuku ya mbolea, ambao umewasaidia wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika shughuli za kilimo.
