Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

News

Afriqom yakutanisha wadau wa tasnia ya mbolea Zanzibar


Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA) kama mdau muhimu wa tasnia ya mbolea nchini imeshiriki kikamilifu katika mkutano wa wadau wa tasnia ya mbolea barani Afrika.Mkutano huo uliokutanisha wadau kutoka nchi 39 za kutoka Bara la Afrika, Asia na Ulaya unaofanyika katika ukumbi uliopo ndani ya hoteli ya Park Hyatt Garden ya mjini Zanzibar kwa siku 3 ambapo siku ya kwanza ulifanyika kwa kutembelea kiwanda cha branding na kufungasha mbolea cha Steinweg Bridge cha Jijini Dar es Salaam.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji wa Ndani na Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja Louis Kasera amepongeza uamuzi wa kufanyia mkutano huo nchini Tanzania nankueleza una manufaa makubwa kwa watanzania na taifa kwa ujumla.Amesema, TFRA ilianzishwa kwa sheria ya mbolea no 9 ya Mwaka 2009 na kuanza kutekeleza jukumu lake la Udhibiti mwaka 2012.Akiwasilisha mada kuhusu Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS), Daniel Maarifa Afisa Biashara Mwandamizi wa TFRA amesema mfumo huo unakutana na changamoto kutokana na wakulima kutokuwa na elimu ya kutosha ya matumizi sahihi ya mbolea na hivyo kutokuona umuhimu wa mbolea kwenye shughuli zao za kilimo.Amesema, kutokana na hali hiyo inawawia vigumu kuagiza mzigo utakawezesha kupata mbolea kwa bei ya chini kwani kiasi kinachoagizwa ni kidogo.Aidha, amebainisha juhudi ymza Serikali ya Tanzania kuhakikisha inatoa elimu ya umuhimu wa kutumia mbolea katika kuongeza uzalishaji pamoja na kutoa ruzuku inayoongeza hamasa ya kutumia mbolea ukilinganisha na ilivyokuwa awali.Afriqom ni kampuni inayojishughulisha na kukusanya, kuchambua na kusambaza takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusu mnyororo mzima wa thamani katika tasnia ya mbolea barani Afrika.