Je nikipoteza namba ya mkulima natakiwa nifanye nini?
Ukipoteza namba ya mkulima piga simu kwenye kitengo cha huduma kwa wateja TFRA 0800110153 au 0800110154 hakikisha una taarifa za muhimu za awali kama kitambulisho namba ya simu ili uweze kurejeshewa namba yako ya mkulima.
