TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania anapenda kuwataarifu walioomba nafasi za kazi ya wawakilishi wa usimamizi wa mbolea za ruzuku ngazi ya Mikoa (Regional Fertilizer Subsidy Representative) na kufanya usaili tarehe 24 -25 Juni, 2023 kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa hapo chini. Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili wanatakiwa kuripoti ofisi za TFRA Dar es Salaam (zlizopo Vetenary karibia na ofisi ya Bodi ya Mikopo) Jumatatu ya tarehe 11/07/2023 saa mbili kamili (2:00) asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za vyeti (Original Certificate) kwa ajiliya taratibu za ajira. Nyaraka zinazotakiwa ni kama ifuatavyo;
i. Vyeti halisi (original certificate) vya masomo kuanzia kidato cha nne, kidato cha sita na chuo kikuu na nakala za vyeti hivyo zilivyothibitishwa na Mamlaka zakisheria (certified by Advocate)
ii. Cheti cha kuzaliwa
iii. Nakala/namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
iv. Picha ndogo tatu za rangi (three colored recent passport size photographs)
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hwakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.