Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
MAFUNZO YA BIASHARA YA MBOLEA –MKOA WA ARUSHA, UKUMBI WA OFISI ZA KANDA CEDHA , TAREHE 6 NA 7 OKTOBA 2026:
04 Oct, 2026

MAFUNZO YA BIASHARA YA MBOLEA – MKOA WA ARUSHA

Ofisi ya TFRA ARUSHA inawatangazia na kuwakaribisha wadau wote kushiriki katika Mafunzo ya Biashara ya Mbolea yatakayofanyika:

📍 Mahali: Ukumbi wa ofisi za kanda CEDHA, Arusha Mjini
📅 Tarehe: 6 na 7 Oktoba 2026
🕑 Muda: Saa 2:00 Asubuhi

Mafunzo haya yanawalenga:

  • Wanaotaka kuanzisha biashara ya mbolea

  • Wafanyabiashara wa mbolea

  • Vyama vya Ushirika

  • Wafanyakazi wa maduka ya mbolea

  • Wafanyakazi wa maghala ya mbolea

Tunawakaribisha wote kujifunza kuhusu taratibu, kanuni na mahitaji muhimu ya kuanzisha na kuendesha biashara ya mbolea kwa usahihi.

OFISI YA TFRA ARUSHA

Karibu ujifunze, uelewe na uanzishe biashara sahihi ya mbolea!