News
Waziri Bashe ataka mbolea kuuzwa muda wa ziada
Tuwawezesha kupata askari watakaolinda eneo la biashara na baadaye kuwasindikiza bank ili waweze kuweka pesa za mauzo zikiwa katika hali ya uhakika na salama.
"Nawaagiza muendelee kuuza mbolea mpaka siku za jumamosi na Jumapili and after working hrs tuongee na askari ili wawepo kuanzia saa 10 na saa 12 wawasindikize bank ili wakaweke pesa za mauzo," Waziri Bashe alisisitiza.
Waziri Bashe ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Januari, 2023wakati wa ziara katika ghala la mbolea la kampuni la ETG ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma.
Aidha, Waziri Bashe alimuagiza meneja wa ETG mkoani humo kufungua vituo vya uuzaji wa mbolea katika maeneo manne ndani ya Wilaya ya Songea ikiwa ni eneo la Mpitimbi, Peramiho, Mgazini na Magagula.
Akitoa maelekezo hayo, waziri Bashe amemtaka meneja huyo kuwasiliana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TRFA) ili kuvisajili vituo hivyo na kuagiza kuwa vifanye biashara kama tawi la kituo cha biashara ETG Songea ( extension ya Songea).
Kwa upande wake Meneja wa ETG Songea Vishnu Vardhan alikiri kupokea maelekezo ya waziri Bashe na kueleza kuwa kufuatia kuwepo kwa uhakika wa usalama wa fedha ya biashara, wapo tayari kuuza mpaka saa 12 jioni.
"Kama utasaidia bank sisi tutaendelea mpaka saa 12 jioni" Vishnu aliongeza.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni la mbolea la Premium, Angelina Haule akitoa uzoefu wake katika utekelezaji wa mpango wa mbolea za ruzuku amesema kufuatia taratibu za kununua mbolea za ruzuku ulivyo, wakulima wanaona wamebanwa na wanapitia hatua ndefu mpaka kupata huduma ikiwa ni pamoja na kumtaka mkulima aliyesajiliwa kwenda mwenyewe kununua mbolea hiyo.
Ameeleza kuwa, kutokana na malalamiko ya wakulima kampuni yake imeendelea kunawatia moyo na kuwataka wavumilie ili kuepusha udanganyifu kufuatia kiasi kikubwa cha fedha kilichotolewa na serikali ili kugharamia ruzuku ya mbolea.