Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

News

Wafanyabiashara 56 wa mbolea kanda ya ziwa wanolewa​


Wafanyabiashara 56 wa mbolea wa kanda ya ziwa wamepewa mafunzo katika maeneo ya sheria ya mbolea, usajili wa mbolea na maombi ya leseni kwa kutumia mfumo wa FIS yaani Fertilizer Information System, aina za mbolea, virutubisho vya mimea, sifa za ghala la mbolea, kanuni za utunzaji wa mbolea, matumizi sahihi ya mbolea na faida zake, athari za matumizi yasiyo sahihi ya mbolea na utunzaji wa kumbukumbu za biashara ya mbolea.
Mafunzo hayo yametolewa na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Ziwa kwa siku mbili yaani tarehe 11 na 12 Mei, 2022 ili kuwajengea uwezo wadau wao katika kujihusisha na biashara ya mbolea nchini.
Aidha, baada ya mafunzo hayo, wadau wa mbolea wametunukiwa vyeti vyenye picha zao ili kuweza kuwabaini pindi masuala ya udhibiti ya mbolea yanapoendelea katika maeneo yao ya kazi.


Wafanyabiashara wa mbolea wakifuatilia mafunzo ya sheria ya mbolea na mfumo wa kidigitali wa mbolea Fertilizer Information System (FIS)

Tanzania Census 2022