Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
Wachezaji TFRA wakabidhi makombe kwa uongozi wa Mamlaka
30 May, 2024
Wachezaji TFRA wakabidhi makombe kwa uongozi wa Mamlaka

Washiriki wa michezo lililoandaliwa na Shirikisho la michezo yaMashirika, Taasisi za Umma na Binafsi (SHIMMUTA) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wamerejea na kukabidhi makombe mawili ya ushindi wa kwanza waliyoyapata wakati wa ushiriki wao katika michezo hiyo.

Akipokea makombe hayo ikiwa ni la ushindi katika mchezo wa pool table na kukimbia ndani ya junia, Mkurugenzi wa TFRA, Joel Laurent ameipongeza timu hiyo na kueleza kufurahishwa na moyo wa kuitetea taasisi kwa furaha na kuhakikisha wanaipa jheshma kubwa.

Amesema amefurahishwa na uamuzi wa Mamlaka na watumishi kujipanga kushiriki michezo hiyo na kueleza TFRA imekuwa miongoni mwa taasisi 53 zilizoheshimu maamuzi ya Serikali ya kuruhusu watumishi kushiriki michezo yenye lengo la kuboresha afya na utendaji wao lakini pia kuwaepusha na kuugua magonjwa yasiyoambukizwa.

Amesema, Mamlaka itajipanga kuhakikisha inaongeza ushiriki wa watumishi katika michezo hiyo kwa kuboresha eneo la watumishi kufanyia mazoezi lakini pia kuboresha bajeti ya michezo ili kufikia adhma ya serikali ya kuhakikisha watumishi wanapata muda wa kufanya mazoezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, Victoria Elangwa ametoa pongezi nyingi kwa ushindi na kueleza kuwa jambo zuri lililofanywa na wawakilishi ni kukaa sehemu moja na kufanya mazoezi kwa pomoja.

“Kitu kizuri walikaa pamoja Mwanguku aliwatafutia sehemu iliyowatosheleza wotwe hivyo ikawa rahisi kujuliana hali na kufanya mazoezi kwa pamoja jambo ambalo ni zuri Sana” Elangwa alimaliza.

Akikabidhi vikombe hivyo kwa uongozi wa Mamlaka huku wakishuhudiwa na watumishi wote wa TFRA Mwenyekiti Msaidizi wa Michezo, TFRA alieleza kuwa Mamlaka ilishiriki michezo ya ndani ijulikanayo kama michezo ya jadi ikiwa ni pamoja na pool table, Kukimbia ndani ya junia, karata, Bao, draft na kurusha vishale.

Ameeleza kuwa, katika michezo yote mamlaka iilifanikiwa kucheza na kufikia robo fainali isipokuwa kwa michezo miwili ilichukua ushindi wa kwanza ikiwa ni mchezo wa pool table pamoja na kukimbia ndani ya gunia na kufanikiwa kurudi na vikombe hivyo huku akiahidi kuongeza makombe mwaka ujao.

“Mwaka jana Mamlaka ilishiriki kwa mara ya kwanza na tulifanikiwa kurudi na ubingwa kwenye mchezo wa pool table ambapo tumetetea kobe na kurudisha tena mwaka huu, lakini pia mwaka huu tumeongeza kombe jingine la kukimbia kwenye junia naamini mwakani tena tutaongeza kombe jingine” Mtambo alimaliza