Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

News

Ubora wa mbolea ni suala la usalama wa nchi: Bashe


Na Mwandishi Wetu,

Suala la ubora wa mbolea ni nyeti na ni suala la usalama wa nchi na endapo , mbolea ya chini ya kiwango ikiingia nchini taifa linaweza kujikukuta linapatamatatizo

Hayo yameelezwa na Nairbu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alipotembelea ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Mhe. Bashe amewataka TFRA kuendelea kudhibiti ubora wa mbolea kwani afya za watanzania zinategemesana usalama wa chakula kinachotokana na utumiaji wa mbolea.

“Tunakokwenda hivi sasa vita vya dunia havitakuwa vya bunduki, bali itakuwa vita vya mitandao na teknolojia ya mbegu na viwatilifu, " alisema Bashe.

Mhe. Bashe ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini kuchukua hatua za kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima pamoja na kuainisha maeneo yenye malighafi ya utengenezaji wa bidhaa hiyo ili kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo.

Mhe. Bashe amesema sekta ya mbolea na viwatilifu ni muhimu katika taifa kwani inaweza kulifanya taifa likawa tegemezi au likawa kubwa ulimwenguni.

Mhe. Bashe aliiagiza mamlaka kuhakikisha inadhibiti bei ya mbolea kwa kupunguza gharama za uzalishaji, usafiri na kuagiza mzigo wa kutosheleza mahitaji wakati bei inapopungua.

"Ninakuagiza Mkurugenzi mkazungumze na TRC na Tazara muingie makubaliano ya kusafirisha mbolea kwenda maeneo mbalimbali nchini” Alisema.

Akitoa mfano Mhe Bashe alisema kuwa mbolea inayoagizwa kutoka nje inafika bandarini kwa Sh38, 000 kwa mfuko, lakini mbolea hiyo ikifika Tunduma inauzwa kwa Sh64, 000 sehemu kubwa ya gharama hizo ni usafiri.

Aliongeza kuwa gunia la mbolea ya tumbaku kutoka Dar es Salaam hadi Tabora kwa lori hugharimu Sh10, 000 wakati kwa treni ni Sh3, 000.

“Gharama hizi za mbolea zinapokuwa kubwa zinafanya gharama za uzalishaji katika kilimo kuongezeka na mkulima kushindwa kushindana sokoni na kuishia kuuza kwa hasara jambo ambalo linakatisha tama”.

Vilevile Bashe aliwaelekeza TFRA kuchangamkia fursa wakati huu ambapo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea kwa kujenga maghala ya kuhifadhi mbolea kandokando mwa reli hiyo kwa kila mkoa ili inapoanza kufanya kazi mizigo ya mbolea iwe inasambazwa katika mkoa husika kutokea hapo.

Kadhalika Bashe aliwaagiza TFRA kushirikiana na Mamlaka ya utafiti wa Kilimo (TARI) kuainisha maeneo yote ambayo malighafi za kutengeneza mbolea zinapatikana ili kuvutia uwekezaji katika bidhaa hiyo inaweza kuzalishwa.

“Kumekuwa na changamoto kubwa ya bei kwa mbolea inayozalishwa hapa nchini, TFRA mnapaswa kukaa kuzungumza na wazalishaji wawaeleze vikwazo vya kikodi vinavyosababisha bei hiyo kuwa juu ili nasi tukajenge hoja kwa wenzetu wa wizara ya fedha ili kuondoa changamoto hiyo ya kikodi," alisema Bashe.

Katika hatua nyingine Bashe aliitaka mamlaka hiyo kuwaza kibiashara katika shughuli zake hususan wakati wa kuagiza shehena za mbolea kutoka nje.

Naibu Waziri aliiagiza TFRAkufuatilia bei za mbolea katika soko la duniamara kwa mara ili waweze kubaini bei inapokuwa imeshuka waweze kuagiza shehena ya kutosha kukidhi mahitaji ya nchi.

Alisema TFRA ikienda kibiashara wakati wa kuporomoka kwa bei ndiyo wakati wa kuingia mikataba na wazabuni kwa kueleza kiwango kinachotakiwa kwa muda fulani huku bei ikiwa ya wakati huohuo.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dk Stephan Ngailo alisema asilimia 90 ya mbolea inayotumika hapa nchini inatoka nje ya nchi na asilimia 10 tu ndio inayozalishwa hapa nchini.Aliongeza kuwampaka sasa mwenendo wa upatikanaji wa mbolea nchini kwa msimu wa 2020/2021 ni wa kuridhisha.

Dk Ngailo alisema makadirio ya mahitaji ya mbolea kwa msimu wa 2020/21 ni i tani 718,051 na mpaka kufikia Novemba 30, tani 506,776 zilikuwa tayari zimeingizwa katika mzunguko.

Dk. Ngailo aliongeza kuwa tasnia ya mbolea inakabiliwa na changamoto mbalimbaliikiwemo gharama kubwa za usambazaji wa mbolea, gharama kubwa za upatikanaji wa mali ghafi za kuzalisha bidhaa hiyo pamoja na kukosekana kwa maabara ya kisasa ya mbolea kwa ajili ya vipimo.