Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
TFRA YAPONGEZWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA MBOLEA LINDI NA MTWARA
29 May, 2024
TFRA YAPONGEZWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA MBOLEA LINDI NA MTWARA

Uongozi wamkoa wa Lindi na Mtwara wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwakuanzisha mashamba ya mfano kwa ajili ya uhamasishaji wa matumizi sahihi ya mbolea katika mikoa hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga katika halfa ya uzinduzi wa mashamba manne ya mfano yaliyolo katika Halmashauri ya Mtama, Ruangwa Masasi na Mtwara Vijijini.

Mhe. Ndemanga amasema uanzishwaji wa mashamba hayo utaleta hamasa kubwa kwa wakulima wa mikoa hiyo kutaka kutumia mbolea katika uzalishaji wa mazao mbalimbali na hivyo kuongeza kipato.

Amesema mikoa ya Lindi na Mtwara ina zaidi ya hekta 6,400, 000 zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali,hatahivy tija ya uzalishaji kwenye mazao mengi bado ni ndogo.

“Takwimu hizi zinaonyesha uwepo wa utajiri wa maeneo ya kutosha yanayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali lakini bado hatujaweza kutumia fursa hii kwa ukamilifu na moja ya sababu ni kwamba wakulima wengi hawazingatii kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi ya mbolea.” Alisema Mhe. Ndemanga.

Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya huyo mikoa ya Lindi na Mtwara kwa miaka iliyopita imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa chakulahivyo kusababisha serikali kuleta chakula cha msaada ili kupunguza kutokea kwa baa la njaa.

Aliongeza kuwa bei za vyakula katika mikoa ya Lindi na Mtwara iko juu ukilinganisha na mikoa mingine nchini na kuwa hii inatokana na uzalishaji mdogo unaosababishwa pamoja na mambo mengine, matumizi hafifu ya mbolea.

Mhe. Ndemanga amesema kwa kutambua mapungufu yaliyopo katika uzalishaji wa mazao mbalimbali mikoa hiyo kwa kushirikiana na TFRA wamezindua mashamba ya mfano katika halmashauri nne ili kutoa elimu kwa wakulima kwa vitendo kuhusu matumizi sahihi ya mbolea.

“Tunawaomba wakulima wote wanaozunguka maeneo ya mashamba ya mfano katika mikoa yote miwili kuchangamkia fursa hii kwa kuangalia manufaa ya matumizi sahihi ya mbolea kwenyekilimo cha mazao ili kuongeza tija katika uzalishaji”,Alisema Ndemanga.

Mhe. Ndemanga amewaagiza maafisa kilimo na maafisa ugani wa Mkoa wa Lindi na Mtwara kuendeleza mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea katika maeneo yao.

Amewaagiza pia wakurugenzi katika halmashauri za mikoa hiyo kutenga bajeti kwa ajili ya kuanzisha, kuendeleza na kugharamia mashamba darasa ya matumizi sahihi ya mbolea kwenye maeneo yao.

Akizungumza mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt. Stephan Ngailo amesema majukumu ya taasisi yake ni pamoja na kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya mbolea.

Dkt. Ngailo amesema TFRA imeanzisha mashamba ya mfano katika halmashauri nne katika mikoa ya Lindi la Mtwara kwa lengo la kuwahamasisha wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na hivyo kuongeza tija na kipato.

Matumizi sahihi ya mbaolea ni pamoja na kujua afya ya udongo kwa kupima udongo wa shamba husika, na katika kutekeleza hili TFRA ilishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele kwa kuchukua sampuliza udongo kutoka katika maeneo yaliyoainishwa na kupimwa katika maabara ya TARI Mlingano, alisema Dkt. Ngailo

Mkurugenzi Mtedaji huyo ameongeza kuwa baada ya matokeo ya vipimo, maeneo manne yalionyesha kuwa yana sifa za kuwekwa mashamba ya mfano na tayari mashamba hayo yameshaandaliwa tayari kwa kupanda ambayo ni Mnolela (Mtama), Chimbila B (Ruangwa), Kitere (Mtwara Vijijiji) na Chigugu (Masasi).

Kwaupande wa pembejeo,Dkt. Ngailo amesema wadau mbalimbali wa mbolea wametoa msaada wa mbolea na mbegu kwa vikundi vya wakulima vinavyoshiriki katika mashamba ya mfano ikiwemo ETG Inputs ambao wametoa (tani 2 za mbolea ), OCP Tanzania Limited

( tani 2 za mbolea ) Premium Ago Chem Ltd(tani 1 ya mbolea ) Wakala wa Mbegu Tanzania - ASA(kilo 50 za mbegu) na ABM Equipments Services LTD (tani moja ya chokaa).

Naye Afisa Kilimo Mkoa wa Lindi akitoa taarifa ya mkoa Bw. Salvatory Kalokola amesema Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye matumizi kidogo ya mbolea nchini kutokana na uelewa mdogo wa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbolea.

Kalokola amesema kuwa matumizi ya mbolea katika mikoa hiyo yamekuwa yakipungua mwaka hadi mwaka na kuongeza kuwa wakulima wanaotumia mboleawengi wao ni wale wanaojishughulisha na kilimo chamazao ya bustani.