Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

News

Pelekeni mbolea vijijini, Naibu Waziri Mgumba awaambia wafanyabiashara


Serikali kupitia wizara ya kilimo imewataka wafanyabiashara wa pambejeo za kilimo ikiwemo mbolea kuweka mawakala wa kuuza pembejeo hizo katika maeneo ya vijijini, kufuatia asilimia kubwa ya mbolea hizo kupatikana kwenye makao makuu ya wilaya na mikoa, hali ambayo inasababisha wakulima kushindwa kuzalisha mazao ya kutosha kutokana na kukosa pembejeo hizo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba katikamaadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Mhe. Mgumba amesema wafanyabishara wengi wako mijini ambapo wateja wao ambao ni wakulima wako vijijini, hivyo ni vema wafanyabiashara hao wakaweka mikakati mizuri ya kuwafikishia mbolea kwa wakati kabla ya msimu wa kilimo kuanza.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Prof. Anthony Mshandeta amesema wakulima wanatakiwa kuacha tabia ya kilimo cha mazoea.

Prof.Mshandeta amesema ili kuongeza matumizi ya mbolea nchini, jitihada mbalimbali zinafanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo. Jitihada hizo ni pamoja na kutoa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari mfano redio, runinga magazeti,vipeperushi namashamba ya mifano.

Katika miaka mitano iliyopitaProf. Mshandeta amesema serikali imeondoa tozo mbalimbali kama vile tozo za leseni za kuuza mbolea na usajili wa mbolea mpya.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mfumo wa BPS na kuondolewa kwa baadhi ya tozo kumechangia kuongeza upatikanaji wa mbolea bora kwa wakati na kwa bei nafuu kwa wakulima.

Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA amesema Mamlakaimekuwa na mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa mbolea ili kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mbolea bora wakati wot na kuongezeka kwa upatikanaji wa mbolea nchini kutoka tani 427,486 mwaka 2015/2016 hadi tani 582,357 mwaka 2019/2020.

Prof. Mshandeta amesema kuwa mafanikio mengine ya TFRA ni pamoja na kuongezeka kwa wazalishaji wa mbolea wa ndani kutoka wanne mwaka2015 nakufikiawazalishaji 12mwaka 2020.

Amesema pia TFRA imefanikiwa kuvihamasisha vyama vya ushirikakushiriki katika ununuzi wa mbolea kwa pamojakupitia mfumowa BPS ambapo katika mwaka huu 2020, Chama kikuu Cha Ushirika cha Wakulima Iringa (IFCU) na Chama cha Msingi Cha Madibira (MAMCOS) vimeshiriki zabuni za BPS na kuingiza mbolea ya kupandia (DAP) na kukuzia (UREA).