Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

News

Kuingiza mbolea kwa mara moja kwa mwaka inawezekana: Bashe


SERIKALI imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na wafanya biashara wa mbolea nchini kuangalia uwezekano wa kuingiza mbolea ya mahitaji ya mwaka mzima kwa mara moja kupitia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa mkulima anapata mbolea hiyo kwa bei nafuu.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alipokuwa akizungumza na wafanya biashara wa mbolea nchini, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) jijini Dodoma hivi karibuni.

Mhe. Bashe amesema uingizaji wa mboleakwa wingi na kwa mara mojakwa mwaka inawezekana, isipokuwa kabla ya kufanya hivyo kuna mambo ambayo serikali pamoja na wadau wa mbolea wanatakiwa kuyatolea ufumbuzi ikiwemonani atagharamia ununuzihuo.

Ili kufanikisha uingizaji wa mbolea kwa wingi na kwa mara moja kwa mwaka, Bashe ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA kuunda kamati itakayo jumuisha TFRA na sekta binafsi waweze kujadili na kuja na mikakati ya namna ya kutekeleza suala hilo lenye lengo la kumsaidia mkulima kupata mbolea bora kwa bei nafuu.

Amesema wakati umefika kwa serikali hususan Wizara ya Kilimo na taasisi zake kutofanya kazi kwa mazoea, badala yake wafikirie kibiashara zaidi na namna ya kumwezesha mkulima kuzalisha kwa tija na kuinua kipato.

Naibu Waziri Bashe amesema, ili kumpunguzia mkulima makali ya bei ya mbolea, TFRA na makampuni ya mbolea wafanyeufuatiliaji wa bei za mbolea kwenye soko la dunia nakuona ni wakati gani zimeshuka ili mbolea iingizwe nchini kwa wingi na kwa mara moja.

Mhe Naibu Waziri ameiagiza TFRA na wafanya biashara wakae pamoja na kujadilinamna nzuri itakayowawezesha kuingiza mbolea kwa wingi kwa mara moka pindi mbolea inapokuwa imeshuka bei katika soka la dunia

“Jambo hili linawezekana; kaeni chini mje na namna bora ya kulitekeleza kwani limewezekana katika nchi nyingine kama Ethiopia na India”,Alisema Naibu Waziri Bashe.

Bw. Hillarykutoka kampuni ya mbolea ya OCP amesema uagizaji wa mbolea kwawingi na mara moja inawezekana isipokuwa serikaliinatakiwa kugharamia uingizaji wa mbolea hiyo kama inavyofanyika nchi zingine.

Aidha Naibu waziri amewaagiza TFRA na wafanyabiasha wa mbolea waangalie uwezekano wa kupunguza gharama za usafirishaji wa mbolea kutoka bandarini hadi kumfikia mkulima katika maeneo mbalimbali nchini.

Ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kusafirisha mbolea kwa njia ya reli ni rahisi kuliko kwa

barabara, hivyo humfikia mkulima kwa bei nafuu.

“Kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea kutoka Dar es Salaam hadi Tabora kwa njia yabarabara ni shilingi 5,500/= wakati kwa njia ya relini shilling 1000/= tu, hii ni tofautiya asilimia sabini”, Alisema Naibu Waziri Bashe.

Kwa upande wa takwimu za mahitaji ya mbolea, Naibu Waziri ameiagiza TFRA kuhakikisha kuwa wanapata takwimu sahihi za mahitaji ya mbolea kutoka maeneo yote nchini ili kurahisisha uagizaji wa bidhaa hiyo.