Diplomasia ya uchumi ya Rais Samia kuibua kiwanda cha mbolea nchini

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Hemed Mwanga amekiri kuwa diplomasia ya uchumi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imekuwa sababu ya kumpata mwekezaji wa kiwanda kikubwacha mbolea cha Intracom Fertilizer Limited kinachojengwa Jijini Dodoma.
Alisema, Rais Samia ni Rais mwenye maono asiyependa kuzungumza na badala yake amejikita katika matendo zaidi.
Mkuu wa Wilaya Mwanga aliyasema hayo jana tarehe 19 Mei, 2022 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kueelimisha wakulima wa eneo la Ilonga wilayani Kilosa Mkoani Morogoro juu ya namna mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho inavyofanya kazi katika kuongeza tija kwenye kilimo.
Kupitia mashamba darasa yaliyopandwa kwa tutumia mbolea itakayokuwa ikizalishwa na kiwanda hicho inayojulikana kama fomi pandia, fomi kuzia pamoja na mbolea iliyozoeleka ya DAP na Urea zimetumika katika mashamba darasa yaliyopo katika scheme ya umwagiliaji wa zao la mpunga ililopo katika kijiji cha Ilonga Kata
ya Chanzulu wilayani Kilosa ili kuonesha utendaji wa mbolea hizo na kuwafanya wakulima wachague mbolea sahihi kwao.
Kufuatia kuwa, mbolea itakayozalishwa kiwandani hapo itakuwa na mchanganyiko wa samadi na kemikali kwa uwiano sawa kutafunguafursa kwa wafugaji kukusanya samadi inayotokana na kinyesi cha ng'ombe na kukiuziakiwanda hicho.
"Samadi sasa hivi ni mali tutapata tenda ya kukusanya samadi na kupeleka kiwandani itazalisha mbolea na mkulimaatatumia mbolea na kupata mavuno mengi yatakouzwanje ya nchi na kutuingizia pesa za kigeni" Mwanga alikazia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Geofrey Mkamilo alisema taifa linamatumaini makubwa na mbolea itakayozalishwa na Itracom Fertilizer Limited katika kutatua changamoto ya upatikanaji na bei ya mboleanchini.
Hata hivyo alisema TARI inaendelea na utafiti wa kuonautendaji wa mbolea hiyo ambapo wanaangalia ulinganifu wa kiasi kinachowekwa kwenye mazao na matokeo yake na baadaye kuwaelezawananchi matokeo ya utafiti huo.
Alisema, pamoja na kujaribu mbolea hiyo katika eneo hilo pia wamefanya katika maeneo mengine nchini.
"Tumeanza kufanyia majaribio ya mbolea hapa Ilonga kwa zao la mpunga, zao la alizeti na mtama homboro, zao la maharage na mahindi eneo la Siriani mkoani Arusha na mkoani Mbeya kwa zao la mahindi, maharage, viazi na mpunga", Dkt. Mkamilo alisisitiza.
Aliendelea kusema, Taasisi anayoisimamia inaendelea na zoezi la kupima afya ya udongo nchi nzima na tayari mikoa 18 imeshapimwa wanaendelea kukamilisha kwa mikoa 8 iliyosalia ili kufahamu udongo una rutuba ya kiasi gani na umepungikiwa na kitu gani kulingana na mahitaji ya zao husika na si kuweka mbolea kwa kubuni tu ili kuwa na kilimo chenye tija.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo alisema kujengwa kwa kiwanda kikubwa cha mbolea nchini kutatatua changamoto ya upatikanaji na bei ya mbolea kwa wakulima.
Aliongeza kuwa utashi wa kisiasa nchini upo vizuri na kutoa wito kwa wawekezaji wengine katika eneo la mboleakuja kuwekeza nchini.
"Malighafi kwa ajili ya kulisha viwanda vya mbolea zipo, nishati ipo, nguvu kazi ipo na soko lipo hivyo wafike kuwekeza" Dkt Ngailo alikazia.
Pamoja na hayo aliwataka waingizaji,wazalishaji na wauzaji wa mbolea nchinikujisajili kwenye mfumo wa ruzuku iliwaweze kushiriki kwenye kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa kiwanda cha Intracom Fertilizer Limited, Nduwimana Nazaire aliwahakikishia wakulima wa Ilonga na Tanzania kwa ujumla upatikanaji wa mbolea na kubainisha kuwa bei ya mbolea itakayozalishwa kiwandani hapo itakuwa nzuri ukilinganisha na aina nyingine za mbolea zinazoingizwanchini kutoka maeneo mbalimbali duniani.
"Msiwe na shida na mashaka mbolea itapatikan…